Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Katika siku za karibuni, zilitangazwa habari tatu kuhusu tatizo hilo sugu la ugaidi nchini Iraq. Habari ya kwanza ni kwamba, kundi la kigaidi la Daesh limemteka nyara Yasir al Jawrani, afisa wa wizara ya mambo ya ndani, ambaye pia ni mkurugenzi wa Idara ya Pasi za Kusafiria ya Al Aadhamiyyah pamoja na marafiki zake watatu katika kitongoji cha Khaaniqin kilichoko mkoani Diyala, kisha likawaua shahidi kikatili na kinyama Wairaqi hao wanne kwa kuwakata vichwa.
Habari ya pili ni kwamba, Sabah an-Nuuman, msemaji wa shirika la kupambana na ugaidi la Iraq amesema, katika mwaka huu uliomalizika wa 2021, kikosi cha kupambana na ugaidi cha shirika hilo kimetekeleza operesheni zaidi ya 300; na katika operesheni hizo, mbali na kutokomezwa maficho ya Daesh, magaidi 100 wa genge hilo la ukufurishaji waliangamizwa na zaidi ya wengine 250 walikamatwa.
Na habari ya tatu ni kuwa, watu wawili waliokuwa na silaha, walitaka kumuua afisa mmoja wa shirika la intelijensia na la kupambana na ugaidi la Addiwaniyah katika eneo la Hayyu-shurtah. Afisa huyo alijeruhiwa katika shambulio hilo la kigaidi na akakimbizwa na kupelekwa hospitali ya Addiwaniyah kwa ajili ya kutibiwa.
Tatizo sugu la ugaidi halikuanza leo nchini Iraq, bali chimbuko lake lilianzia tangu miongo miwili nyuma. Kwa hakika ugaidi ni matokeo ya siasa za Marekani kuhusiana na Iraq. Kusambaratisha miundomsingi ya kijeshi na kiusalama ya Iraq ni matunda ya siasa na sera zilizotekelezwa na Mareani katika nchi hiyo.
342/